Wednesday, 8 December 2010

Ninawezaje kufahamu mapenzi ya Mungu juu ya maisha yangu?

ya maisha yangu? Biblia inasemaje juu ya kuyajua mapenzi ya Mungu?




Swali: "Ninawezaje kufahamu mapenzi ya Mungu juu ya maisha yangu? Biblia inasemaje juu ya kuyajua mapenzi ya Mungu?"

Jibu:
Kuna njia mbili za kukuwezesha kujua mapenzi ya Mungu katika wakati unapokabiliana na hali fulani (1) hakikisha kile unachotakakukifanya hakikukatazwa na biblia. (2) hakikisha kile unachotaka kukifanya kitaleta utukufu kwa Mungu na kukusaidia kukua kiroho. Kama haya mawili ni sawa nab ado Mungu hakupatii kile unachokiomba basi si mapenzi ya Mungu upate kile unachokiomba. Unahitajika kusubiri tena kwa wakati kidogo.mapenzi ya Mungu wakati mwengine huwa ni magumu. Watu hutaka Mungu awaambie cha kufanya- Afanye kazi wapi,aishi wapi, aoe nani, na kadhalika. Warumi 12:2 inatuambia, “msifanane tena hali ya ulimwengu huu, lakini mbadilishwe kwa kufanywa upya kwa dhamira zenu. Nanyi mtaweza kujaribu nakutambua mapenzi ya Mungu- mapenzi yake mema ya kupendeza.”

Mungu mara chache sana hutoa habari zake moja kwa moja. Mungu hutuachia nafasi ya kujichagulia. kile Mungu hataki sisi tufanye ni dhambi au kupinga mapenzi yake. Mungu hutaka tufanye uamuzi sawa na mapenzi yake. Na sasa utajuaje mapenzi yake juu yako? Ukiwa unatembea karibu na Bwana na huku ukitamani kwa bidii kufanya mapenzi yake maishani mwako- Mungu atakuwekea mapenzi yake moyoni mwako. Njia ni kutaka mapenzi ya Mungu, si yakobinafsi “furahi katika Bwana naye atakupa mapenzi ya moyo wako” (Zaburi 37:4). Kama biblia haipingi na kitu hicho kinaweza kukufaidisha kiroho- basi biblia inakupa ruhusa kufanya uamuzi na kufuata yaliyomo moyoni mwako.

No comments:

Post a Comment